Asilimia 27 ya Wanawake Tanzania wanafanya ngono kinyume na Maumbile RIPOTI YA (NIMR )YADAI zaidi soma hapa


Asilimia 27 ya Wanawake Tanzania wanafanya ngono kinyume na Maumbile RIPOTI YA (NIMR )YADAI zaidi soma hapa

  

Mwandishi wa BBC John Solombi ameripoti kwamba utafiti mpya unaonyesha asilimia 27 ya wanawake Tanzania wanafanya ngono kinyume na maumbile.

Mtafiti Mwanasayansi Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya watafiti wenzake wa NIMR amesema katika utafiti walioufanya umebaini asilimia 26.5 ya wanawake hukubali kuingiliwa kinyume

Sababu: Wanawake - kujiongezea kipato, kukwepa kupata mimba, kulinda ubikra (wa kuma) na mila. Wanaume: Raha, kukwepa UKIMWI.

Baadhi ya wanawake kutoka Kinondoni Dar es salaam, Tanga, Makete na Siha wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile ambapo Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
Amekaririwa akisema “ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo
Wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambapo Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.
Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ni hafifu kwani wakitumia mipira (Condom) inapunguza raha.
Wanawake pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana akiolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo likichukua nafasi.
Watafiti hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana, wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili kusukuma mtoto. 
habari hii kwa msaada wa blogu nyingine.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget