WEMA SASA AHAMIA KWA PASTOR, AMUHARIBIA SIKU PASTOR MYAMBA, SOMA SABABU YA KUFANYA HIVYO HAPA

STAA wa filamu mwenye jina kubwa
nchini, Wema Sepetu hivi karibuni
alimuharibia siku Emanuel Myamba
maarufu kama Pastor Muyamba, kwa
kushindwa kufika kwenye hafla iliyokuwa
imeandaliwa na chuo chake cha sanaa
‘TFTC’ akiwa kama mgeni rasmi.

Wema Sepetu.
Mtoa habari wetu ndani ya taasisi hiyo
aliliambia gazeti hili kuwa, Wema
aliombwa na kukubali kuhudhuria shughuli
hiyo, lakini alipopigiwa simu dakika za
mwisho aliwaambia kwamba atashindwa
kufika kwa kuwa amefiwa na shangazi yake
udhuru ambao baadaye ulibainika kuwa
haukuwa wa kweli.

Alisema kutokana na kutofika kwa staa
huyo, ambaye hata hivyo mwaliko wake
ulitokana na shinikizo la wanafunzi wa
chuo hicho, walilazimika kuwaomba radhi
wageni wengine, wakiwemo waandishi wa
habari.

Emanuel Myamba 'Pastor Muyamba'.
Mmoja wa watu wa karibu na Wema

aliliambia gazeti hili kuwa muigizaji huyo
hajawahi kupatwa na msiba siku za hivi
karibuni, kwani mara zote amekuwa
akiwaeleza kila linapotokea jambo zito
kama hilo.

Mtu huyo alisema katika ratiba ya siku
hiyo, walikuwa waende kwenye tukio moja
la starehe na halikuwa limebadilika.
juzi alipoulizwa Pastor Myamba alikiri
Wema kutofika kwenye hafla hiyo kitendo
alichosema kimemsikitisha kwani walitoa
mwaliko kwake kutokana na heshima
aliyonayo.

“Nimemshangaa sana, lakini mbona
mwenzake Jokate alikuja, ni kwa sababu
anajitambua na ni professional,” aliema
Myamba.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget