1. Ukienda kwake ukutane na
vyombo vichafu na nguo chafu
zimejazanausidhani ni mvivu, ni
kamtihani anakupa.
2. Ukiingia kwake ukaona
anampigia simu yule dada wa
usafi anayekujaga mara moja kwa
wiki aje afanye usafi alipwe
usidhani eti anajali kihivyo.
Anakutest aone kama utasema
"Acha baby, ntakufulia mpenzi
wangu".
3. Ukikuta kwake amefanya
shopping ya vyakula vya kupika
kama unga, mchele, na vingine
halafu akakwambia mwende ule
mgahawa fulani mkapate dinner
usidhani eti ana hela kibao ya
kutumia! Anakutest aone kama
utamwambia mbaki kwake mpike
mle. Uko chumba cha mtihani!
4. Siku kakuahidi kukutoa out
halafu unafika kwake unakuta
kajikunyata kama mgonjwa
anakwambia mama ake kapiga
simu anaumwa anaomba atumiwe
hela. Halafu anakwambia hela
aliyo nayo na ukipiga mahesabu
unaona ni kama ile ya kutumia
mkiwa out. Anakuomba ushauri
afanyaje. Wewe unamwambia
"Baby twende out, suala la mama
nina uhakika kaka zako na dada
zako watalishughulikia,
atawapigia". Woiyeeee! My sista
hapo umejimaliza!!
5. Ukimtembelea kwake ukakuta
anapika na kufanya usafi wewe
Umekaa tu unaangalia muvi halafu
ukitaka umsaidie anakwambia
endelea kuangalia muvi karibu
anamaliza na wewe kweli ukarudi
ukakaa kuendelea na muvi yako!
Siku zako zinahesabika!!
6. Ulishawahi kumwambia mpenzi
wako aende kwenye ibada?
Alipokataa ulimsisitizia? My sister,
hata walevi wanapenda wanawake
ambao wanawasisitiza kwenda
kwenye ibada. Sio tule wale kila
siku wanashinda baa na club.
7. Mara ngapi huwa
unamkumbusha kuwapigia simu
wazazi au ndugu zake kuwajulia
hali mkiwa wote? Angalao akupe
na simu na wewe uwasalimie? Huo
ni mtihani mwingine huwa mnafeli
sana.
8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza
kabla ya ndoa. Sio kila saa
ukimtembelea ni kujiachia tu.
Inaleta adabu na inawafanya
mkazanie kufikia lengo kubwa la
maisha.
9. Jaribu ukiwa unaenda kwake
uwe unaenda na tuvitu kama
nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote
huwa wanaume ni shida kununua
mara nyingi.
10. Wakati mwingine nenda kwake
hata na CD za dini mpelekee
msikilize. Sio kila ukifika kwake
wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne
na kina nani sijui. Ukiwa hivyo
hataona tofauti kati yako na wale
macho juu anakutana nao club
kila wikiendi.
11. Jenga na tabia ya kumnunulia
tuzawadi tudogo tudogo.
Sometimes unakuja na boksa au
kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa
wanaume inaonyesha unaweza
kujipa majukumu na kuyasimamia.
Marks hizo.
IMEANDIKWA NA MASSANJA
MKANDAMIZAJI
Post a Comment