KWA WALE WAPENZI WA MARA CLARA HUU NDO ULIKUWA MWISHO WAKE,, gerry hakufika mwisho na ukatili wake,, fuatilia.



Clara amemfungulia MARA na kutoroka, lakini Gary anafika na na kumuuliza Clara kwanini amemfungulia MARA? Lakini akiwa bado ameshikilia bastola na hasila za kufa mtu, polisi wanafika.
Gary anafanikiwa kukimbia  na kuruka ndani yam to na kuwachenga polisi. Tayari Clara ameanza kumsaliti baba yake “Gary” kwa kumfungulia MARA. Lakini pia Clara huyo huyo anamsaliti Gary baada ya Gary kumpigia simu huko alikofanikiwa kutorokea akimtaka Clara aongozane nae ili wakapande boti watoroke kusikojulikana.
Lakini Clara anaanza kukumbuka usemi wa MARA aliomwambia kipindi cha nyuma kuwa “Gary anataka tu akutumie kama chambo ili ampate mama (Alvira)”. Baada ya Clara kuwaza hivyo, anaamua kwenda hadi kwa akina MARA na kuanza kutubu mbele ya MARA huku akijutia yote aliyomfanyia tokea mwanzo.
Baada ya Gary kugundua kuwa Clara amemsaliti kwa kwenda kuwaambia akina AMANTE mpango wa Gary kutaka kutoroka naye, sasa Gary anaamua kumpigia simu Clara na kumpa vitisho “kwakuwa umeamua kunisaliti , wakati wewe ndiye niliyekuwa nibebakia na wewe, upendo wangu woote nilikupatia, sasa maisha yako yote yatakuwa ya shida” alisema Gary.
Usiku Alvira akiwa kwake kupitia dirisha lake anamuona mtu akinyemerea nje ya nyumba yao, Alvira anamuita mumewe “Amante” kwa sauti kubwa “Amante!! Amanteee!! Namante anawapigia polisi simu. Polisi wanafanikiwa kumkamata mtu huyo, lakini mtu huyo alikutwa na kibox kidogo na alisema kuwa kunamtu alimuagiza akifikishe kwa Alvira.
Ndani ya kibox kulikuwa  na bonge la pete pamoja na Ujumbe wa malavidavi ambao kumbe Gary ndiye aliyeuandika ili umfikie kipenzi chake Alvira. Alvira anausoma na kujikuta akimuuliza mumewake Ujumbe huu unamaana gani!?.
Baada ya kuona kasha kasha za Gary zinazidi kuchukua sura mpya, Alvira na Amante wanaamua kumchukua MARA na SUZAN na kuwakodishia gari ili iwatoroshe kuwaokoa na balaa za Gary. Wanapanda gari, wakiwa safarini wanasinzia wote wakimuacha dereva akiendesha. Mara ghafla mbele ya safari, Gary anaonekana ndiye dereva wa lile gari, ile MARA na Suzan wanashtuka kuuliza dereva, Gary anashuka na kuwafungulia mlango, wanapigwa na butwaa!!!.
Gary anawateka na bastora na kuwaamuru waingie katika jengo moja linalotisha kinyama, Gary anaamua kumwambia MARA kuwa yeye ndiye chanzo cha maisha yake kuharibika nayeye ndiye aliyesababisha  mdogo wake Cairlo afariki dunia, na tokea MARA akizaliwa alikuwa kikwazo ndio maana akafanya mipango wakabadilishwa na Clara ili Clara apate maisha mazuri.

Wakati huo Suzan ni mja mzito lakini Gary anamsukuma hadi chini wakiwa na MARA, baada ya unyama wa Gary kuzidi MARA anamwambia Gary “yani huna hata huruma kwa mwanao aliyeko tumbini? Gary anamfuata Suzan kwa upole na kumwambia kuwa  unamtoto tena? Mimi ninaye mtaka ni Alvira na Clara tuu!
Gary anamchukua MARA na kumfungia ndani ya Tanki la maji na kufungulia maji huku akirudishia mfuniko. Maji yanazidi kujaa, wakati gary akiwa nje Amante, Alvira na Clara wanawasili huku Amante akiwa ameshikilia bastola. Mpango ulikuwa hivi, Gary alimtaka Clara aletwe ili wabadilishane na MARA.
Walipofika Gary anamuamuru Amante aweke basola chini ili kumnusuru mwanae MARA.Amante mara baada ya kuiweka chini Gary anaishika na kumkabidhi Alvira na kumuambia bila kupoteza muda muuwe mumeo ili umuokoe MARA, ukishindwa atakufa. Alvira anachukua bastora na kumnyooshea Gary. Gary na kumuambia “ ukiniripua utamkosa MARA”. Alvira naamua kijinyooshea bastola yeye mwenyewe ili ajiuwe, lakini Gary anamshika mkono na kuanza kujibizana, lakini ile Gary amegeuka, Amante alijaribu kumpora bastola.
Wakati seke seke likiendelea, huko MARA maji tayari yamekwisha mfunika hadi juu ya kichwa, lakini Clara nafanikiwa kwenda kumtafuta MARA. Anafika alikofungiwa MARA,anaona chini cheni ya shingoni ya MARA ikiwa nchini, anapata wazo la kufunua tanki la maji na kumkuta MARA ndani yake, anamuokoa.
Amante anaikosa bastola na Gary kufanikiwa kumtupa chini ya ghorofa hilo. Gary anamrudia Alvira  lakini anakosea na kumshuti mwanae CLARA hadi chini. Ile anataka kumshuti Alvira, Suzan anatoka kwa nyuma  akiwa amebeba bonge la chuma na kumtandika kichwani, ile bado anataka kumshuti Alvira, SUZAN anamchoma GARY chuma tumboni na kumuua, lakini kabla hajafa alifanikiwa kumuambia mama yake kuwa “mama nakupenda, nakumpenda sana” baada ya maneno hayo alikata roho. Siku iliyofuata SUZAN alijifungua watoto mapacha na wote walioigiza Tamthilia ya MARA CLARA walionekana wote kwa pamoja wakipata picha ya ukumbusho, isipokuwa Gary hakuwepo.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget