Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea
uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini kama mbaya zaidi kuwahi kuonekana
duniani na kuyataka mataifa ambayo yaliahidi kutoa msaada wa zaidi ya
dola millioni mia sita kutoa fedha hizo.
Limeonya kuwa vita vinavyoendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi huenda vikasababisha baa la njaa nchini humo.
Shirika la chakula duniani WFP limesema kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa watoto elfu hamsini huenda wakapoteza maisha yao kutokana na utapia mlo mwaka huu huku thuluthi moja ya raia wakikabiliwa na na viwango hatari vya njaa.source bbc
Post a Comment