Israel yashambulia Ghaza licha ya makubaliano

Israel imeendelea kuushambulia Ukanda wa Ghaza licha ya kuafiki kusitisha vita huku idadi ya Wapalestina wanaouliwa shahidi katika mashambulizi ya utawala huo ikiwa imefikia 900. Wapalestina wasiopungua 20 wameuawa shahidi leo Jumamosi katika shambulio moja la anga la Israel katika mji wa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Ghaza. Ashraf al Qidra msemaji wa Wizara ya Afya ya Ghaza amesema kuwa, wahanga wa shambulio  hilo wote walikuwa ni watu wa familia moja wakiwemo watoto wadogo kadhaa.
Mbali na kuaawa shahidi Wapalestina hao wasiopungua 20, Mpalestina mwingine mmoja amefariki dunia hii leo huko Bait-lahiya kutokana na majeraha makubwa aliyokuwanayo. Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya siku 19 ya utawala haramu wa Israel imefikia 900 huku kukiwa na majeruhi wasiopungua 5,700. Umoja wa Mataifa kwa upande wake umesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya vifo huko Ghaza ni vya raia wa kawaida wakiwemo watoto zaidi ya 200.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget