Usitishaji vita kwa masaa 12 waanza Ghaza

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/dc04b17cde1ff3f9c3d620e505e430ea_XL.jpg

Usitishaji vita kwa  masaa 12, umeanza katika eneo la Ukanda wa Gaza, baada ya muqawama kukubaliana na pendekezo hilo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, usitishaji vita huo, umeanza saa 05: 00 kwa wakati wa Ghaza. Hatua hiyo imekuja huku watu 900 wakiwa wameuawa shahidi na wengine zaidi ya elfu sita kujeruhiwa. Idadi ya mashahidi imeongezeka na kufikia 900 baada ya shambulizi jingine la utawala huo mapema leo asubuhi dhidi ya familia moja ya Najjar katika eneo la Khan Yunus, kusini mwa ukanda huo ambapo watu 14 wameuawa shahidi. Shambulizi hilo limefanyika ikiwa ni kabla ya kujiri utekelezwaji wa usitishaji mapigano. Hii ni katika hali ambayo jeshi la utawala huo limetangaza kuuawa askari wake wengine wawili na kujeruhiwa wengine 14 hapo jana usiku kufuatia mashambulizi ya wanamapambano wa Palestina.sourse iran

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget