TAIFA STAR YAKIONA CHA MOTO

Usiku wa November 17 watanzania wengi na
wapenzi wa soka walikuwa wakisubiri kuona
mchezo wa pili wa marudiano wa kuwania
kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi kati ya timu
ya taifa ya Algeria dhidi ya timu ya taifa ya
Tanzania Taifa Stars , mchezo ambao ulihezwa
Blida Algeria katika uwanja wa Mustapha
Tchaker .
Taifa Stars ambayo lionesha kiwango kizuri
katika uwanja wa nyumbani Dar Es Salaam licha
ya kulazimishwa sare ya goli 2-2, wameshindwa
kutamba katika mchezo wa pili na kukubali
kipigo cha goli 7-0, ilichukua dakika 45 za
kwanza Taifa Stars kuanza kuruhusu magoli
matatu ya mwanzo, magoli ambayo yalianza
kukatisha tamaa wa Tanzania .
Wakati Taifa Stars wanatafakari namna
ambavyo watasawazisha magoli Mudathir
Yahaya alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 41,
kipindi cha pili kocha wa Tanzania Boniface
Mkwasa alifanya mabadiliko ya kumuingiza Aishi
Manula na kumtoa golikipa Aly Mustapha na
Farid Mussa nafasi yake ikachuliwa na Salum
Telela , mabadiliko ambayo hayakuzaa matunda.
Magoli ya Algeria yalifungwa na Yacine Brahimi
dakika ya 1, Faouzi Ghoulam dakika ya 23 na
dakika ya 59 akapachika goli jingine kwa mkwaju
wa penati, Riyad Mahrez dakika ya 43 na Islam
Slimani kafunga kwa mkwaju wa penati dakika
ya 49 na 75, Carl Medjani dakika ya 72 . Kwa
matokeo hayo Taifa Stars imetolewa kwa jumla
ya magoli 9-2 baada ya mchezo wa awali
kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget