Wasifu wa Edward Lowassa

Edward Ngoyai Lowassa anatoka katika ya jamii
ya wafugaji Kaskazini mwa Tanzania.
Alizaliwa August 26 mwaka 1953 kijijini Ngarashi
Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.
Kitaaluma Lowasa ni msomi , akiwa na shahada
kwanza kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam na
shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Bath
huko Uingereza (1983-1984).
Uzoefu katika siasa
Edward Lowasa ni mtoto wa tatu wa Mzee
Ngoyayi.
Ingawa baba yake alikuwa mfugaji aliwahi pia
kufanya kazi kama tarishi katika serikali ya
wakoloni.
Alijiunga na chama cha CCM mara tu baada ya
kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka wa
1977.
Kabla ya kugombea ubunge , aliwahi kutumikia
jeshi la Tanzania na hata kupigana katika vita
kati ya Tanzania na Uganda vilivyopelekea Idd
Amin kuondolewa madarakani.
Baada ya hapo alikuwa mtumishi wa umma kwa
miaka kadhaa kabla kuteuliwa kuwa mbunge
kuwajilisha vijana na kujiunga rasmi na siasa.
Mwaka wa 1990 alijitosa ulingoni kugombea
nafasi ya ubunge katika jimbo la uchaguzi la
Monduli.
Alifanyikiwa kwa miaka yote hii Lowassa
ameendelea kulishikilia jimbo hilo la uchaguzi
hadi sasa anapolazimika kuliachia ili kuwania
Urais.
Hii si mara yake ya kwanza kugombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kwani
mwaka 1995,alikuwa miongoni mwa watangaza
nia 15, hata hivyo nafasi ikachukuliwa na
Benjamin William Mkapa.
Hata hivyo tofauti na matarajio ya wafuasi wake,
Mwaka 2005, Lowassa hakuwania nafasi hiyo,
badala yake aliunga mkono rais anayemaliza
muda wake Jakaya Kikwete.
Je Lowassa huyu wa sasa amewahi kuwa nani
katika nyadhifa alizozipitia kiserikali?
Edward Ngoyayi Lowassa amewahi, kuwa Waziri
wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Ardhi na
Maendeleo ya Makazi pamoja na nafasi
nyinginezo.
Lakini pia nafasi za juu alizowahi kuzipata ni
pamoja na kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka Febuari 7
mwaka 2008, alipolazimika kujiuzulu baada ya
madai ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa ya
Kampuni ya Richmond, Madai ambayo bwana
Lowassa aliyakanusha hadi sasa.
Katika siasa,Lowassa anafahamika kama mtu
wenye misimamo mikali,kwa kile anachokiamini
mwenyewe kama siasa zinazo ambatana na
maamuzi magumu.
Licha ya kuwa mwanachama wa CCM kwa miaka
38, bwana Lowassa aliwashangaza wanachama
wa CCM kwa uamuzi wake wa kukihama chama
hicho.
Hatua iliyochangiwa na yeye kutoridhrishwa na
jinsi uteuzi wa wagombea urais wa kilichokuwa
chama chake ulivyoendeshwa.
Alijiunga na chama cha kikuu cha upinzani cha
CHADEMA.
Hiki ni mojawapo ya vyama vinne vya upinzani
vinavyounda umoja uitwao,UKAWA.
Kufuatia uamuzi wake wa kubadili chama,
Edward Lowasa amelazimika pia kubadili
msimamo wake wa kisiasa na kuwa mpinzani wa
chama tawala na sera aliziunga mkono na
kuzitumikia awali, jambo ambalo linawatatanisha
wakosoaji wake .
Hii ni mara yake ya pili kujaribu kuingia ikulu.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget