Hii ni mipango mingine ya milionea Aliko Dangote huko Zimbabwe…

Mwananume tajiri  kuliko wote Africa, Aliko Dangote anaziandika headlines zake kwenye kurasa za biashara na uwekezaji barani Africa. Baada ya kuweka wazi mipango alionayo juu ya Tanzania time hii ameweka wazi mipango mingine alionayo juu ya nchi zingine za Africa.
Safari hii ni zamu ya Zimbabwe kukamata fursa zinazoletwa na Dangote nchini kwao… Tajiri Dangote ameweka wazi mipango yake ya kuwekeza dola million 400 (Billion 800 za Tz) kwenye ujenzi wa kiwanda kikubwa cha simenti nchini humo.
dangote3
Aliko Dangote na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Aliko Dangote aliweka wazi mipango hii siku ya Jumatatu akiwa kwenye press conference na waandishi wa habari jijini Harare baada ya kukutana na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na Makamu wa Rais  Emmerson Mnangagwa.
>>“Tumeamua kuwekeza ndani ya Zimbabwe, ndio maana tupo hapa. Nchi yoyote utakayoona tunaitembelea inamaanisha, ndio, tumeamua kuwekeza hapo.” <<< Dangote aliwaambiwa waandishi wa habari wa Harare.
dangote4
Aliko Dangote na mwanae Halima kwenye sherehe ya Times 100 Gala jijini New York Marekani.
Mipango mingine aliyonayo juu ya Zimbabwe ni pamoja na uwekezaji wa uchimbaji madini na uzalishaji wa umeme nchini humo. Kama serekali ya Zimbabwe ikitoa kibali basi ujenzi wa kiwanda hicho utanza mwaka 2016 na ujenzi utakapoisha kiwanda hicho kitakuwa kinazalisha tani milioni 1.5 za simenti kwa mwaka.
                                             sourse millardayo.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget