Idadi ya shule zilizoungua kanda ya kaskazini yaongezeka

Headlines za baadhi ya mabweni ya shule kuungua katika mkoa wa Arusha na manyara imekuwa ikiendelea ambapo katika mkoa wa Arusha jeshi la  polisi kupitia kwa kamanda Charles Mkumbo aliviambia vyombo vya habari kwamba kwa Arusha mpaka sasa hivi ni mabweni ya shule sita  ndio yaliyoungua.

Aidha idadi ya shule ambazo zinakuwa zimekumbwa na matukio hayo iliongezeka Jana August 29 2016 ambapo bweni la shule ya Aldasgate wilayani babati mkoani manyara limeungua, tukio hilo limekuwa ni la pili kwa mkoa wa manyara. Kamanda wa polisi Manyara Fransis Jacob amesema……….

>>>’Bweni moja liliwaka moto na hivyo kuteketeza baadhi ya vitu vya wanafunzi lakini kwenye vyumba hivyo viliweza kuokolewa lakini baadhi, kama asilimia 80 ya vitu viliweza kuokolewa, bado tunafanya uchunguzi kujua chanzo chake
Tukio hilo la shule ya Aldasgate linafanya matukio ya kuungua kwa shule kwa kanda ya kaskazini kufikia nane ndani ya kipindi kifupi.source milladrayo

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget