Soko la kilombero hatarini kwa magojwa ya mlipuko

M kuu wa soko la kilombero jijini Arusha bi Lucy Bungi ametoa wito kwa mkurugenzi wa halmashauru kurejea mkataba waliosaini na kampuni ya live stork demonstration kwa ajili ya kufanya usafi sokoni hapo kwani kampuni hiyo imeshindwa kazi na endapo watabaini ukweli waweze kuuvunja mkataba huo.
 
Akitoa malalamiko ya uchafu wa mazingira sokoni hapo bi Bungi alisema kuwa soko la kilombero kwa sasa limekidhiri kwa  uchafu jambo ambalo linnatia hofu kwa wafanya biashara wengi kufanya biashara kwa wasiwasi wakiofia magonjwa ya mlipulo sokoni hapo
 
Bi bungi aliwatupia lawama wakala wa usafi kutoka kwenye kampuni husika na usafi sokoni hapo na kusema kuwa kampuni imeonyesha dhairi kwamba imeshindwa kazi jambo ambalo limepelekea yeye mwenyewe kama mkuu wa soko kusimamia usafi ndani ya soko jambo ambalo ni nnje ya majukumua yake,
 
Kutokana na malalamiko hayo jitiaza za chombo hiki zilifanikiwa kukutana na msimamizi wa usafi sokoni kutoka kwenye kampuni hiyo bwana Simbano Kimbute ambae alikanusha madai hayo na kusema kuwa kampuni haijashidwa kufanya kazi  kwani hali ya soko kwa sasa inaridhisha japo siyo kwa kiwango kinachohitajika kwani wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi ikiwemo diwani wa kata ya levolosi bwana Nanyaro kuwakataza wafanyabiashara kulipa ushuru jambo lililochangia baadhi ya mazingiza kuwa mabovu
 
Kutokana na madai hayo kuelekezwa kwa diwani chombo hiki kilifanikiwa kuzungumza nae ambapo diwani Nanyaro alikubali kwamba yeye ndiye aliewakataza wafanya biashara kulipa ushuru kutokana na sababu anazozifahamu peke yake na kuahidi kutobadilisha kauli hiyo kwa wafanya biashara mpaka pindi atakapo jiridhisha yeye mwenyewe,
 
``kuwakataza wafanyabiashara kulipa ushuru  kusiwe sababu ya mazingira machafu`` Alisema diwani Nanyaro huku akiwatupia lawama wakala wanaohusika na swala la usafi sokoni hapo.
Hata hivyo chombo hiki kimebaini kuwa kuna tofauti kubwa katika uongozi wa soko dhidi ya wakala wa usafi sokoni hapo na endapo swala hilo halitafanyiwa ufumbuzi huenda magojwa ya mlipuko yakalikumba soko la kilombero kwa sasa..

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget