Afisaa mmoja wa polisi
mwanamke nchini Kenya amepewa
onyo kali kwa kuvalia sketi
iliyokuwa imembana kiasi cha
kuonyesha umbo lake.
Wakuu wake walichukua hatua ya
kumuonya polisi huyo baada ya
picha yake kusambazwa kwenye
mitandao ya kijamii na kupigiwa
gumzo kubwa.
Alipigwa picha akiwa amevalia
sketi yake fupi na yenye kumbana
akiwa anashika doria katika eneo
ambako mashindano ya magari
yalikuwa yanafanyika eneo la Kati
mwa Kenya.
Post a Comment