Baada ya Diamond Platnumz kuchomoa kiasi
cha Dola 25,000 sawa na Tsh millioni 40 za
kitanzania kwa director Clarence Peters wa
Nigieria kwa ajili ya kufanya production ya
video ya number one remix aliyomshirikisha
Davido ambapo ilijumuisha gharama za kila
kitu hadi models na dancers , sasa jamaa
ameamua kuchomoa mpunga huohuo yaani
Dola elfu 25 kwa director MoE Musa ambae
anaishi na kufanya kazi zake nchini Uingereza
kwa ajili ya video yake mpya aliyomshirikisha
Iyanya kutoka nchini Nigeria.
Gharama hizo za Dola elfu 25 ($25,000)
hazitajumuisha gharama za kumsafirisha
Iyanya kutoka Nigeria pamoja na malazi na
kila kitu anapokua nchini Uingereza. Kwasasa
Diamond Platnumz yupo nchini Ghana
ambapo anategemea kufanya kolabo nyingine
na Davido itakayowahusisha pia Tiwa Savage
wa Nigeria na Mafikizolo wa South Africa
ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha
TV barani Afrika
props : vibe
Post a Comment