Wapenzi wengi wa filamu duniani watakuwa
wanalitambua jina lake ambapo kwa
Tanzania ni maarufu zaidi uswahilini lakini
duniani ndio anatajwa kuwa muigizaji
anayejulikana zaidi.
Jina lake ni Shahrukh Khan ambae ni
mwigizaji wa filamu kutoka India ambapo
jana ametengeneza headlines baada ya
kutajwa na jarida la maswala ya fedha la
Wealth-X la Singapore ndio mwigizaji tajiri
zaidi Asia pia anashika nafasi ya pili duniani
nyuma ya comedian Jerry Seinfeld ambaye
ana utajiri wa dola za kimarekani milioni
820.
Khan ambaye ni maarufu kwa jina la Kingh
Khan ana utajiri wa $600m akiwa kawazidi
waigizaji wakubwa Hollywood kama Tom
Cruise mwenye $480 million, akiwafuatia na
Johny Depp na Tyler Perry ambao wote wana
$450 million.
Listi hiyo imechanganya waigizaji washindi
wa tuzo za Academy kama Jack Nicholson
($400 million), Tom Hanks ($390 million) na
Clint Eastwood ($370 million) Nicholson ni
namba 6 akifuatiwa na Hanks, Bill Cosby,
Eastwood na Adam Sandler.
Stori kama hizi ni halali yako zisikupite…. ili
niwe nakutumia kila kinachonifikia ungana na
mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA,
kama upo Facebook na Instagram pia
unaweza kubonyeza FB na INSTA ili kupata
kila stori inayonifikia zikiwemo videoz, vituko,
pichaz, music na mengine yote.
Post a Comment