
Headline nyingine ya leo Tanzania kuhusu dawa za kulevya imetokea Bungeni Dodoma ambapo Waziri William Lukuvi aliwasha kipaza sauti baada ya maswali ya mbunge Anne Kilango Malecela.
Alianza kwa kusema ‘Baada ya Wafanyabiashara wa dawa za kulevya kukamatwa na dawa hizo ambapo uchunguzi ukishakamilika Watuhumiwa hufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kushitakiwa Mahakamani kwa mujibu wa sheria, dawa za kulevya zilizokamatwa huifadhiwa na kutumika Mahakamani kama vielelezo na baada ya kesi kukamilika dawa hizo huaribiwa au kuteketezwa kwa amri ya Mahakama’
‘Uteketezaji wa dawa za kulevya umewahi kufanyika mwaka 2012 ambapo kilo tisini na mbili (92) za Heroine ziliteketezwa katika kiwanda cha Saruji Tanga ziliteketezwa kwa amri ya Mahakama na mwaka 2013 kilo mia nne kumi na mbili za bangi na kumi na mbili za Heroine, kilo tano nukta sita za Cocaine ziliteketezwa kwenye kiwanda cha Saruji Wazo Hill Dar es salaam’

Maelezo ya Waziri Lukuvi yanaendelea ambapo kwenye hii sentesi ya tatu amesema ‘zoezi la kuteketeza dawa za kulevya ni shirikishi na hufanyika chini ya usimamizi wa taasisi mbalimbali kama tume ya kuratibu udhibiti wa dawa za kulevya, jeshi la Polisi, Mahakama, ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali, baraza la taifa la usimamizi wa mazingira, Waandishi wa habari na taasisi nyingine husika’
‘Serikali imeshaandaa muswada wa sheria mpya kali zaidi itakayo ondoa changamoto zilizokua zikijitokeza wakati wa matumizi ya sheria iliyokua inatumika sasa, muswada wa sheria hii mpya utawasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano huu unaoendelea’ – Lukuvi

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu William Lukuvi akasimama na kuibu kwa kusema ‘kwa niaba ya Mh. Waziri Mkuu, ni kweli sheria hii inayotumika sasa ina upungufu mkubwa na kesi zinachukua muda mrefu sana ikilinganishwa na nchi za wenzetu kama Bangladesh, sijakwenda lakini nimesoma kwamba kwenye viwanja vyao vya ndege wameweka hata vituo na hakimu wa zamu anakuwepo palepale Airport, akikamatwa mtu anaitwa hakimu wa zamu anatoa hukumu kazi inaisha’
‘Kwa sheria yetu hii hata ukimuona mtu na dawa za kulevya haitoshi mpaka ziende kwa Mkemia mkuu alafu upelelezi ufanyike, tunazo baadhi ya hukumu mbalimbali zimetolewa vibaya pengine kutokana na sheria iliyopo, matatizo tuliyonayo yote ni kwa sababu ya sheria hii’kwa hisani ya millardayo.com
Post a Comment