
Rais John Dramani Mahama wa Ghana ambaye mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS jana aliongoza ujumbe wa jumuiya hiyo nchini Burkina Faso ili kusaidia mpango wa kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia, baada ya jeshi kumteua afisa wa ngazi za juu kuongoza nchi hiyo. Ujumbe huo uliojumuisha Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria na Macky Sall wa Senegal umefanya mazungumzo na Luteni Kanali Isaac Zida, vyama vya upinzani, wafuasi wa Compaore, viongozi wa kidini na makundi ya kiraia. Mahama amesema kwamba makundi yote yametakiwa kuchagua wagombea watatu kwa ajili ya uteuzi wa rais wa mpito na kwamba kipindi cha serikali ya mpito kitakuwa cha mwaka mmoja.
Post a Comment