Hatimaye Kenya na Tanzania zimeafikia suluhu ya mgogoro uliokuwa
ukiendelea kuhusu agizo lililotolewa kwa kampuni ya ndege ya KQ kupunguza
safari zake za ndege nchini Tanzania.Kwa sasa ndege za Kampuni ya KQ kutoka
Kenya zitaendelea na safari zake kama ilivyokuwa huku magari ya utalii ya
Tanzania yakiruhusiwa kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi.Viongozi wa mataifa haya mawili Jakaya Kikwete na mwenzake Uhuru
Kenyatta waliafikiana katika mkutano nchini Namibia
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa
mambo ya nje wa Tanzania Bernald Membe amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya
viongozi hao wakuu wa nchi hizo mbili kukutana nchini Namibia walikokwenda
kuhudhuria maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Namibia.
Makubaliano ya marais hao yanakuja siku chache
baada ya mzungumzo ya mawaziri wa utalii wa Tanzania na Kenya kuvunjika
mwishoni mwa wiki kufuatia pande hizo mbili kushindwa kufikia muafaka kuhusu
magari ya Tanzania yaliyopigwa marufuku uwanja wa Jomo Kenyatta.
Post a Comment