Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Agosti, 2016
amemteua Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Kabla ya uteuzi
huo Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango
(Sera).
Bw. Doto M. James
ataapishwa kesho tarehe 01 Septemba, 2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Kufuatia uteuzi
huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius
Likwelile atapangiwa kazi nyingine.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
Salaam
Post a Comment