Wanawake 60 watoroka mikononi mwa Boko Haram

Zaidi ya wanawake na wasichana sitini waliokuwa wakishikiliwa kwa zaidi ya wiki mbili na wanamgambo wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, wamefanikiwa kutoroka huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Kiongozi mmoja wa kieneo katika mji wa Maiduguri makao makuu ya jimbo la Borno amesema kuwa, karibu wanawake na wasichana 63 siku ya Ijumaa walifanikiwa kutoroka mikononi mwa wanamgambo wa Boko Haram na kurejea kwenye makazi yao. Kiongozi huyo amesema kuwa, wanawake hao walifanikiwa kutoroka mahala walipohifadhiwa wakati wanamgambo hao walipokuwa wakipambana na majeshi ya serikali. Taarifa kutoka Maiduguri zinasema kuwa, wanamgambo 50 wa Boko Haram waliuawa siku ya Ijumaa baada ya kujiri mapigano kati yao na majeshi ya serikali ya Nigeria katika kitongoji cha Bambwa. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la Boko Haram bado lingali linawashirikilia wanafunzi wa kike wapatao 267 wa shule ya Chibok, waliotekwa nyara tokea mwezi Aprili uliopita.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget