Mutharika asisitiza kupambana na umasikini Malawi


 Mutharika asisitiza kupambana na umasikini Malawi
 Rais Peter Mutharika wa Malawi amesema kuwa, umasikini ni adui mkubwa zaidi nchini humo. Akizungumza kwenye sherehe za kutimia miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo, Rais Mutharika amesisitiza kuwa serikali yake inalipatia kipaumbele suala la kupambana na umasikini. Rais wa Malawi ameongeza kuwa, kutopiga hatua za kimaendeleo na utegemezi wa misaada ya madola ya kigeni, ndiyo mambo makuu mawili yaliyodumaza uchumi wa nchi hiyo. Matamshi ya Rais wa Malawi yanatolewa katika hali ambayo, takwimu rasmi zinaonyesha kuwa, karibu nusu ya wananchi wa nchi hiyo wanaishi chini ya mstari wa umasikini, huku nchi hiyo ikigubikwa na kashfa ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma. Mwishoni mwa hotuba yake, Rais Peter Mutharika ametaka uwepo umoja na mshikamano kati ya viongozi na wananchi kwa shabaha ya kukabiliana na wimbi la ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget