Watu 29 wauawa kwenye machafuko mapya Kenya
Kwa akali watu 29 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa, baada ya
watu wanaobeba silaha kufanya mashambulio katika maeneo mawili tofauti
katika Kaunti za Lamu na Tana River, Pwani ya Kenya. Mwenda Njoka
Msemaji wa Wizara ya Usalama wa Ndani wa Kenya amesema kuwa, wanamgambo
wanaobeba silaha walilishambulia eneo la Hindi, lililoko umbali wa
kilomita 15 kutoka Kaunti ya Lamu na kuuawa watu tisa. Njoka ameongeza
kuwa, watu wengine 20 waliuawa kwenye shambulio lililofanywa katika eneo
la Gamba lililoko karibu na Kaunti ya Tana River. Wakati huohuo,
Abdulaziz Abu Musab Msemaji wa al Shabab amesema kuwa, kundi hilo ndilo
lililohusika na shambulio hilo. Kwa upande mwingine William Ruto Naibu
wa Rais wa Kenya amevitaka vyombo vya usalama kuwasaka na kuwatia
mbaroni watekelezaji wa shambulio hilo. Hayo yanajiri katika hali
ambayo, Grace Kaindi Naibu Inspekta wa Jeshi la Polisi la Kenya
amelituhumu kundi la Mombasa Republican Council MRC kuwa ndilo
lililohusika na shambulio hilo ambalo linatajwa kuwa linalotokana na
msukumo wa kisiasa, kidini au mgogoro wa ardhi.
Post a Comment