WHO: Ebola imeua watu 518 Magharibi mwa Afrika

 WHO: Ebola imeua watu 518 Magharibi mwa Afrika
Shirika la Afya Duniani WHO limeripoti kuwa idadi ya watu waliofariki dunia kwa homa ya ebola huko magharibi mwa Afrika imefikia 518. WHO ilieleza jana Jumanne kuwa, kesi mpya 50 za homa ya ebola zimeripotiwa kugunduliwa huko Guinea, Liberia na Sierra Leone kuanzia Julai 3 hadi 6. WHO pia imeashiria kuwa, watu wengine 844 wanashukiwa kuambukizwa homa hiyo ya ebola. Guinea ni nchi ya magharibi mwa Afrika iliyoathiriwa vibaya na homa ya ebola ikiwa na watu 408 walioambukizwa homa hiyo huku wengine 307 wakiwa tayari wameaga dunia. Hadi sasa hakuna tiba ya ebola, homa ambayo dalili zake ni kutapika, kuharisha na kuvuja damu.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget