Kupatwa kwa jua au Annular Eclipse hutokea pale jua na mwezi zinapokuwa kwenye mstari mmoja ambapo umbo la mwezi linaonekana kuwa dogo zaidi kuliko umbo la jua.
Wanayansi wanasema kwamba September 1, 2016 Tanzania ndio itakuwa sehemu pekee ambayo kupatwa huko kwa jua kutaonekana vyema na kuwavutia watalii wengi.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya Uingereza imeripoti kwamba kupatwa huko kwa jua kutaanza kwenye bahari ya Altantic, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Msumbiji, kisiwa cha Madagascar kisha kwenye Bahari ya Hindi.
Wataalamu wanasema kwamba miongoni mwa maeneo yatakayoonekana vizuri kwa kupatwa kwa jua ni Mbeya na Tunduru, Ruvuma ambapo tukio hilo litachukua dakika 3 hadi dakika 7.
Post a Comment