Rais Macky Sall wa Senegal jana mjini Nairobi alikagua reli
inayounganisha mji huo na ule wa pwani wa Mombasa na reli hiyo itasaidia
kuhimiza maendeleo ya uchumi barani Afrika. Rais Sall amesema reli hiyo ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya Afrika na China kwenye ujenzi wa miundombinu ya kisasa, na inaendana na matarajio ya Afrika ambayo ni kuboresha miundombinu ili kuhimiza biashara na ushirikiano wa kikanda na maendeleo ya viwanda.
Rais Sall ametoa wito kwa nchi za Afrika kuimarisha uhuisano na China, ili kuhimiza mabadiliko ya kiuchumi na kijamii barani humo.sourse cri
Post a Comment