Matokeo Marekani 2016: Trump amshinda Clinton uchaguzi wa urais

Hillary Clinton and Donald TrumpDonald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.
Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake.
Bw Trump alikuwa ameshinda majimbo mengi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.
Alikuwa ameshinda Ohio, Florida, na North Carolina, ingawa Bi Clinton alishinda Virginia.
Kwa sasa Trump ana kura 265 za wajumbe na Clinton 218 kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.
Lakini mgombea wa Republican Bw Trump ameshinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.
source bbc news

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget