Timu ya taifa ya Tunisia
Kama ilivyotabiriwa, vigogo hao walishambuliana vikali wakati wa mechi hiyo, lakini juhudi za kufungana ziliambulia patupu hadi dakika za mwisho pale Youssef Msakni alipovurumisha kombora kali kutoka zaidi ya mita ishirini hadi kimnyani.
Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu na hadi kufikia mapumziko hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Mshambulizi wa Algeria baada ya kukosa bao la wazi
Kufuatia ushindi huo Tunisia sasa inashikilia nafasi ya pili na alama tatu sawa na Ivory Coast iliyoiilaza Togo kwa magoli 2-1 katika mechi ya awali ya kundi hilo, lakini inadunishwa na idadi ya magoli.
Algeria ni ya tatu huku Togo ikivuta mkia bila alama yoyote.
Katika timu 16 zinazowania Kombe la Mataifa ya Afrika, ni timu mbili tu zilizopata ushindi baada ya kucheza mchezo mmoja kila moja.
Timu hizo ni Mali iliyoifunga Niger bao 1-0 katika kundi B na Ivory Coast kuicharaza Togo magoli 2-1 kwenye kundi D. Timu hizo sasa zina pointi 3 kila moja.
Mechi zaidi za makundi
Mashambiki wa Tunisia waliofika kushuhudia mechi hiyo
Afrika Kusini ina pointi 1, baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Cape Verde katika mechi ya ufunguzi, huku Angola nayo ikitoka sare ya aina hiyo ilipomenyana na Morocco.
Katika kundi hilo hilo, Morocco itakuwa ikikabiliana na Cape Verde. Kwa sasa kila timu ina nafasi ya kusonga hatua ya robo fainali.
Post a Comment