"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu
nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba
maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu likawa huru
alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi.
Alinifundisha.
Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya
nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama haikutosha
sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu
mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa
msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi
huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tutumie kinga lakini
aliipinga sana.
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini
alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa
mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye
atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa
tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea
kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale.
Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na nyingine kidogo.
Nikazoea lakini nikawa na wahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia
jambo baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na
maumbile. Alinilawiti!! Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa
kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo
hiyo ni mbinu mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume
wangu. Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo
ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali
sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo.
Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema
ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile.
Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto.
Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi?
Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!! Nilijuatayari
ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima
hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia.
Siku
zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana.
Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo
akajitambulishanyumbani na alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha
yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba
mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini
niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.
Nikaambiwa
kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya
kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa.Nililia sana huku nikimkumbuka
yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu sahihi.
Nimekuandikia baruahii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie
wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana
wa kileo wanaodanganyikanakufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao.
Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie
vibayamaana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote
kuhusu yule mume mdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya
wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa
sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia
wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume
mwenzako
Post a Comment
mungu tusaidie