Ni utaratibu wa izabreez.com kila wiki kuzileta kwako pichaz za nyumba za kisasa kutoka kwenye kona mbalimbali ikiwa na lengo la kukufungua macho na kuona wengine wamejipangaji kwenye sehemu wanazoishi.
Unaweza ukawa hauna uwezo wa kujenga nyumba kama hii lakini ukawa na uwezo wa kurekebisha chochote unapoishi mfano garden, madirisha, sebule, jiko, mpangilio kama wa meza, chumba na vitu vingine vingi.
Huwa wengine wanachukulia poa swala la taa lakini ukiziweka ovyo ni moja ya makosa makubwa kwenye ujenzi, taa ndio uhai wa nyumba wakati wa usiku…. ni aidha zitapendezesha nyumba au kuharibu kama hukuzipangilia vizuri.
Hii nyumba ipo Mexico City huko Mexico.