Mwandishi Jeny Edward anayeripoti kituo cha TVI hapa Arusha amegeuka
mwiba kwa viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini wakiwemo mawaziri,kwa
kuwakwida wampatie fedha wanapokuwa kwenye ziara mbalimbali za kikazi
huku akitumia kivuli cha kuwafanyia interview.
Mfano halisi ni juzi waziri mkuu,Mizengo Pinda alipokuwa kwenye
kongamano la nyuki jijini Arusha,bila aibu akiwa na mwenzake alimfuata
hadi chumbani alikofikia katika hotel moja maarufu hapa mjini na
kumlazimisha ampatie fedha huku akimweleza kuwa yeye hakulipwa kwenye
mkutano huo.
Kana kwamba haitoshi waziri Nyalandu naye alipata joto hilo hilo kwa
kufuatwa kwenye sehemu ya kupumzikia katika jengo la mikutano AICC
akitakiwa ampatie fedha ,Nyalandu pamoja na kujitetea kuwa hawezi kutoa
hela hadharani ,alilazimika kuongozana na mwandishi huyo hadi kwenye
gari lake na kumpatia mshiko wake.
Mimi kama afisa habari wa wizara nilisikitishwa sana na tabia hiyo
hasa baada ya kuelezwa kuwa ndiyo tabia yake iliyojengeka ya kuwaomba
fedha mawaziri,najua hii tabia ipo sana hapa Arusha lakini nimeambiwa
huyu ndo kinara wao ,naomba chama cha wanandishi wa habari Arusha APC
walishughulikie suala la maadili jambo hilo sio jema,mbaya zaidi
alimwagia matusi ya nguoni mbele yangu mwakilishi wa habari na maelezo
wa mkoani Arusha, Prisca Libaga baada ya kumfuata na kumhoji tabia ya
kuwazonga viongozi hadi kwenye magari akitaka wampatie fedha.hisani jamiiForum
Post a Comment