Marekani yawafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi


Obama 
Rais Obama ameamuru kutimuliwa kwa wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi kutaka kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.
Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae kuwekewa vikwazo.

Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti washtushwe na vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.
Kwa upande wake, rais mteule mara kwa mara amekuwa akizipuuzia taarifa hizo za udukuzi, lakini hivi amesema atakutana na wakuu wa mashushu wa Marekani ili kulijadili hilo. 

Urusi nayo imekana tuhuma za kufanya udukuzi mfumo wa mtandao wa chama cha Democratic.
Msemaji wa serikali ya Urusi amesema Urusi nayo italipiza kwa kiwango hicho hicho.
SOURCE:BBC SWAHILI

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget