Baada ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds TV na
kuwalazimisha watangaza wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi
kinachomuhusu Askofu Gwajima kikiwa hakijamaliziwa maandalizi kinyume na
taaluma ya habari, Leo March 22, 2017 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
limefanya kikao cha maamuzi dhidi suala hilo.
TEF pamoja
na Club ya Waaandishi wa Habari Dar es saalam (DCPC) na Umoja wa Club
za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) zimepitisha maamuzi matatu
ikiwemo.
- Kulaani vikali vitendo vya RC Paul Makonda
- Kutoandika na kutangaza habari zozote kuhusu Paul Makonda kwenye chombo chochote cha Habari.
- Kumtangaza RC Makonda kama adui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na yeyote atakayeshirikiana naye.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.