Blaise Compaoré, aliyekuwa rais wa Burkina Faso, ameondoka Côte d'Ivoire .
Aliyekuwa
rais wa Bukina Faso, Blaise Compaoré ameondoka Côte d'Ivoire na
kujielekeza Morocco. Blaise Compaoré ameondoka na familia yake, Ikulu ya
Abidjan imethibitisha.
Blaise
Compaoré alikimbilia Yamoussoukro Oktoba 31, siku alipojiuzulu. Ikulu ya
Abidjan imesema Blaise Compaoré anaruhusiwa kuingia na kutoka katika
aridhi ya Côte d'Ivoire.(P.T)
Mapema
Jumatano jioni Novemba 19, chama cha CDP cha Blaise Compaoré kiliomba
radhi kwa kukosa kubwa kiliyofanya la kutaka kufanya marekebisho ya
Katiba, jambo ambalo lilizua maandamano na ghasia hadi kupelekea rais
Blaise Comaporé kujiuzulu, na kukimbilia katika mji wa Yamoussoukro
nchini Côte d'Ivoire
Wakati
huohuo rais wa mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando amemteua Jumatano
Novemba 19 luteni kanali Isaac Zida kuwa Waziri mkuu.
Awali luteni kanali Yacouba Isaac Zida alisema yuko tayari kushikilia wadhifa wa Waziri mkuu iwapo atateuliwa.
Awali luteni kanali Yacouba Isaac Zida alisema yuko tayari kushikilia wadhifa wa Waziri mkuu iwapo atateuliwa.
Luteni
kanali Yacouba Isaac Zida anatazamiwa kwa upande wake kuunda baraza la
mawaziri 25 ndani ya saa 72, kukabiliana na changamoto ambazo rais wa
mpito, Michel Kafando, alizibainisha siku ya Jumanne Novemba 18 wakati
wa kuapishwa kwake na ambaye anatumaini kuwa wananchi wa Burkina Faso
watachangia kikamilifu kutatua matatizo hayo.
Uteuzi wa
luteni kanali Yacouba Isaac Zida umezua hisia tafauti, baadhi
wamekaribisha uteuzi huo, huku wengine wakiwemo baadhi ya wanadiplomasia
wa kigeni wakipinga kuona mwanajeshi akishikilia wadhifa wa Waziri
mkuu.
Rais wa
mpito, Michel Kafando aliteuliwa Jumanne Novemba 18 kuwa rais kwa muda
wa mwaka mmoja, kupitia makubaliano yaliyoafikiwa na wadau wote katika
mgogoro uliyokua ukiendelea nchini Burkina Faso, baada ya maandamano ya
raia kuangusha utawala wa Blaise Compaoré.
" Nataka
kuwaambia kwamba nimepokea majukumu haya kwa heshima kubwa, lakini pia
kwa unyenyekevu mkubwa", rais mpya wa mpito alisema katika hotuba yake
ya kwanza aliyoitoa Jumanne Novemba 18. Rais Michel Kafando aliongeza
kwamba "unyenyekevu wa mtu unaonekana pale anapoheshimu muda wa madaraka
anaopewa kwa kipindi cha mpito, unyenyekevu wa mtu pia ni kufahamu
kwamba cheo ni dhamana".
Post a Comment