Mpenzi
msomaji wangu, unapojaaliwa kuwa na mafanikio jambo la kwanza unatakiwa
kumshukuru sana Mungu pamoja na wale ambao kwa namna moja ama nyingine
wamekufanya ufike hapo ulipo.Huwezi kufanikiwa kwa ujanja wako,
mafanikio yako yote nyuma yake kuna mkono wa Mungu. Yeye ndiye anayeweza
kuziona jitihada ulizonazo na akaona akutimizie ndoto zako.
Ukiacha
yeye, wapo watu mmojammoja au kwa vikundi na taasisi ambao wamechangia
wewe kuwa na mafanikio uliyo nayo. Hawa ni watu wa kuwaheshimu sana.
Kamwe usiwasahau, endelea kuwa nao karibu kwani umuhimu wao kwako ni
mkubwa sana.
Aidha,
unapofanikiwa na wewe unatakiwa kuwa chachu ya mafanikio kwa wengine.
Unatakiwa kuwashika mkono ndugu, marafiki na watu wengine wanaokuzunguka
ili watoke kwenye hali duni walizonazo. Ukifanya hivyo utazidi kupaa
kimafanikio na hata siku moja huwezi kuporomoka.(P.T)
Ipo
mifano mengi ya watu ambao wamefanikiwa lakini wanakosa furaha kuwaona
watu wanaowazunguka bado wanaogelea kwenye dimbwi la umasikini.Hawa
utawaona wakiwa mstari wa mbele kuwasaidia wengine kimawazo na hata
kifedha ili nao wainuke na waweze kutimza ndoto zao.
Iko wazi
kwamba bosi wangu, Eric Shigongo ni miongoni mwa watu wenye mafanikio
makubwa. Kama uliwahi kusoma popote kuhusu historia ya maisha yake,
utaona ni jinsi gani amepambana kufika hapo alipo.
Kinachotia moyo zaidi ni kwamba, licha ya mafanikio aliyonayo, hajaridhika, bado anaendelea kupambana na kuzidi kujiwekea malengo makubwa zaidi.(P.T)
Kinachotia moyo zaidi ni kwamba, licha ya mafanikio aliyonayo, hajaridhika, bado anaendelea kupambana na kuzidi kujiwekea malengo makubwa zaidi.(P.T)
Lakini
licha ya mafanikio yake, bosi wangu huyu ambaye pia ni mwalimu wa
ujasirimali amekuwa akitumia muda wake mwingi kutoa elimu kwa watu
mbalimbali juu ya namna wanavyoweza kutoka kwenye umaskini na kuingia
kwenye utajiri.
Amekuwa
akifanya hivyo kupitia vitabu vyake, kwenye makongamano na semina
mbalimbali akieleza njia ambazo yeye amepita mpaka akafikia hapo alipo
sasa. Ukiacha elimu anayotoa, pia amekuwa akiwasaidia wengi kifedha ili
waweze kutimiza ndoto zao. Hiki ndicho ambacho watu waliofanikiwa
wanatakiwa kukifanya.
Huwezi
kuendelea kuwa kwenye mafanikio kama utakuwa mchoyo wa kuwafanya na
wengine wafanikiwe. Utakuwa ni mtu wa ajabu kama utakuwa unataka
ufanikiwe wewe tu na wengine waendelee kuwa mafukara.
Hivi
utakuwa ni mtu wa aina gani kama una pesa nyingi lakini umekuwa mgumu
kuwasaidia wale ambao wanahitaji msaada kutoka kwako? Faida ya wewe
kufanikiwa ni ipi sasa kwa jamii yako?Mimi nadhani kuna kila sababu ya
wale ambao wamefanikiwa kuona wana jukumu la kuwasaidia na wengine
kufanikiwa.
Kama si kwa kuwapa mitaji basi hata kwa kuwapa mawazo ambayo yanaweza kubadili fikira zao.
Usijenge mazingira ya kwamba wewe tu ndiye unayestahili kuishi vizuri, wasaidie na wengine waishi maisha ya furaha. Kumbuka faida ya kufanya hivyo ni kubwa sana.
Usijenge mazingira ya kwamba wewe tu ndiye unayestahili kuishi vizuri, wasaidie na wengine waishi maisha ya furaha. Kumbuka faida ya kufanya hivyo ni kubwa sana.
Kwanza
Mungu atakuongezea mafanikio yako na utashangaa kila unalolipanga
linatimia. Pia, jamii inayokuzunguka itakupenda na itakuona ni mtu
unayejali wengine.
Kwa maana
hiyo unapofanikiwa usijitenge na jamii inayokuzunguka. Saidia pale
inapopidi, washike mkono wengine waweze kusimama. Kumbuka siku wakiwa
wamefanikiwa, ile tu kusema ‘flani kanisaidia mimi kufika hapa’, Mungu
anakuzidishia baraka na unashangaa mambo yanazidi kukunyookea.
Post a Comment