Baadhi ya wajumbe waliyokuwa tume ya mabadiliko
ya katiba wameitaka serikali ichapishe kwa wingi na kuzisambaza kwa wananchi nakala
za katiba pendekezwa, ili wananchi waisome na kuielewa kabla ya kuipigia kura
ya maoni.
Wakizungumza katika
mdahalo ulioandaliwa na mfuko wa MWALIMU
NYERERE
uliofanyika JIJINI DAR ES SALAAM,
wajumbe hao akiwemoaliyekuwa mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu JOSEPH
SINDE WARIOBA, wameelezea kutoridhishwa na tunu za taifa haki
za makundi mbalimbali kama vile watu wenye ulemavu, wanawake na watoto pamoja na baadhi ya vipengele kuondolewa,
Akizungumza katika mdahalo
huo, aliyekuwa mjumbe wa tume BW HAMFREY POLEPOLE
ametaka kuwepo maridhiano ya kikatiba kati ya pande mbili za muungano ili uwepo
muungano unaokubaliwa, unaodumishwa na kulindwa kikatiba huku akieleza
kusikitishwa na kitendo cha kufutwa kwa ibara muhimu zilizokuwa katika rasimu ya
katiba na kushauri ibara hizo zirejeshwe kwani ndiyomsingi wa katiba inayozingatia
maslahi ya wananchi na taifa imara.
Hata hivyo mdahalo huo umekuwa na ulinzi mkali wa polisi tofauti na midahalo mingine ambapo mwandishi alishuhudia wahudhuriaji wakiwa wanakaguliwa na vifaa maalum kabla ya kuingia ndani.,
Post a Comment