KKKT WAPATA PIGO,ASKOFU THOMAS LAIZER WA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI AFARIKI DUNIA
Habari zilizotufikia hivio punde kutoka Jijini Arusha zinaarifu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Ask Thomas Laizer amefariki dunia.
Taarifa hizo zinadai kuwa Ask. Laizer amefikwa na umauti alasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha.
Jana Februari 6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini kati. habari na izack mwacha..
Post a Comment