Mamilioni ya Wanachama cha Ushirka Manushi Sinde yazolewa na Viongozi wa Chama.


Na Izack Mwacha, Kilimanjaro. 0756494796
Viongozi wa chama cha ushirika manushi sinde mkoani Kilimanjaro watuhumiwa kwa kosa la kuzoa mamilioni ya fedha za mradi wa biashara ya wanachama na kujinufaisha wenyewe huku wakijua kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria,
Akizungumza katika mkutano wa hadhara ukiofanyika mwanzoni mwa wiki hii katika ofisi ya chama manushi sinde mwenyekiti mpya wa chama hicho Bwana John Boshe alisema kuwa bodi ya chama kilichokuwepo madarakani mwaka 2011 ilitimia kwa matumizi binafsi  jumla ya shilingi milioni saba  70,00000 za wanachama zilizokuwa zimetengwa kama mtaji wa biashara ya vinywaji kwa ajili ya chama kwa ujmla.
Jambo hilo lilizuka baada ya mwenyekiti huyo aliyeko madarakani kwa sasa kufungua mkutano  na kusoma Agenda ya Mkutano Huo, Ambapo Agenda kuu Ilikuwa ni Kusoma mapato na matumizi ya Msimu uliopita, na hapo walibaini kuwa bodi iliyopita Inadaiwa fedha za wanachama ambazo zilitumika kwa matumizi ya watu binafsi.
Aidha bwama Boshe alifafanua kuwa katika mkutano wa bodi uliopita Viongozi hao walikubali kwa Barua maalum kuwa Wamehusika na Utumiaji usiohalali wa Fedha hizo na kuahidi kwmba watazirejesha lakini mpaka sasa ni mkutano mpya wa bodi nyingine nab ado hawajazirejesha fedha hizo.
Pia bodi iliyohusika na matumizi ya fedha hizo walitajwa katika mkutano huo Ambapo mwenywkiti Alikuwa ni Paul Kiria, Katibu ni Domitila Antoni, pamoja na viongozi wengine Ambao ni Ruben Hugo, Aloyce Joseph, Josephati Wiliam, Edmond malania, Pamja na Thomas masswe,
Kwa upande wake Afisa Ushirika ambaye ni mshauri wa Vyama hivyo Bwana Jorge Robert alisema kuwa Viongozi hao wameonyesha  Dharau na Kiburi kikubwa kwa wanachama kwani hakuna hata mmoja wao aliyehudhuria mkutano huo na kuongeza kuwa  jambo hilo linatakiwa lipelekwe kwa Mrajisi Mtendaji wa Vyama Vya Ushirika ili atumie vipengele vya sheria kuzirejesha fedha hizo kwa wanachama.
Katika mkutano huo ukiohudhuriwa na Wanachama zaidi ya (150) Wote kwa ujumla wao Waliadhimia na Ushauri wa Afisa  Ushirika na kukubali kupeleka swala hilo kwa Mrajisi msaidizi wa Vyama Vya Ushrika ili aweze kutumia vipengele vya sheria vilivyowekwa kusimamia Utendaji wa vyama ili Fedha hizo ziweze kurudshwa mikononi mwa Wanachama..

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget