VITI MAALUMU VYAFUTWA, UBUNGE KUWA NA UKOMOVITI MAALUMU VYAFUTWA, UBUNGE KUWA NA UKOMO



Tume ya Mabadiliko ya Katiba imependekeza katika rasimu ya Katiba Mpya ukomo wa wabunge na kufutwa kwa nafasi za Viti Maalumu bungeni.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Joseph Warioba alisema jana, wanapendekeza kwamba ubunge uwe na ukomo wa vipindi vitatu vya miaka mitano, mitano akimaanisha kwamba kipindi cha mtu kuwa mbunge hakiwezi kuvuka miaka 15.

Rasimu hiyo ya Katiba imependekeza kutokuwapo tena kwa Viti Maalumu na badala yake, imetaka kuwapo kwa nafasi tano za uteuzi zibaki kwa Rais ambazo zitahusisha makundi maalumu ya watu wenye ulemavu pekee.

Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa
majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75. source: jambo tanzania

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget