MATAJIRI 5 MAARUFU BONGO WALIOKUTANA NA OBAMA

WAFANYABIASHARA watano wakubwa (matajiri) Tanzania walikutana na Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama Jr na kufanya mazungumzo ya pamoja katika ziara ya kiongozi huyo barani Afrika iliyofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita na mwanzoni mwa mwezi huu.

Tanzania ina wafanyabiashara wakubwa wengi ambao wana fedha zao na mali za uhakika, lakini hao watano ndiyo waliopata bahati ya kuonana uso kwa uso na rais huyo na kuongea naye.
Mkutano wao ulifanyika Julai Mosi, saa 1:23 usiku kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro iliyopo Barabara ya Kivukoni Front, jijini Dar es Salaam.

Orodha ya majina ya wafanyabiashara hao na makampuni yao kwenye mabano ni kama ifuatavyo:
Said Salim Bakhressa (Mkurugenzi Mtendaji wa Bakhressa Group), Reginald Abraham Mengi (Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media Group), Ali Mfuruki (Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment  Group).

Wafanyabiashara wengine waliokuwa miongoni mwa wafanyabiashara hao wa Afrika ni Mahesh Patel (Mwenyekiti Mtendaji wa Export Trading Group) na Susan Mashibe (Mkurugenzi Mtendaji wa Tanjet).

Wafanyabiashara wengi kutoka mataifa mengine Afrika walihudhuria, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Kenya alihudhuria James Mwangi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, wengine waligoma kuja Bongo kwa madai kuwa Obama alipaswa kwenda  kuonana nao nchini mwao na si Tanzania.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget