KIONGOZI WA WAFANYAKAZI AUAWA AFRIKA.

marikana 79e3f
Afisaa mmoja wa chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa migodini (NUM) ameuawa kwa kupigwa risasi katika mgodi wa madini wa Marikana nchini Afrika Kusini ambako wachimba migodi wengine 34 waliuawa na polisi mwaka mmoja uliopita.
Wanachama wenzake wamesema kuwa mwanamke huyo ambaye ni muuza duka aliuawa asubuhi ya leo.
Wanachama wa chama cha (NUM) wametaja mauaji hayo kama mabaya sana na kusema kuwa wameghadhabishwa mno..
Uhasama kati ya vyama vya wafanyakazi, katika mgodi huo umesababisha kuuawa kwa wafanyakazi kadhaa katika mwaka mmoja uliopita.
Haijulikani ikiwa mauaji ya leo yanahusishwa na mzozo uliopo sasa kati ya vyama hasimu vya wafanyakazi.
Chama cha NUM kimesema kuwa kimekasirishwa na polisi kutopiga hatua katika kuwakamata wahusika kwa kile walichosema ni mauaji ya kupangwa katika mgodi wa Marikana.
Msemaji wa Lonmin, Sue Vey, aliambia shirika la Reuters kuwa polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza mauaji hayo.
Mauaji yaliyotokea mwaka jana mwezi Agosti yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu Afrika Kusini kupata uhuru.,chanzo. mjengwa blog

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget