Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki(EAC),Bi Jesca Eriyo amewataka vijana katika nchi za Afrika ya Mashariki,kuchangamkia fursa zilizopo katika ukanda wa afrika ya mashariki ili kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na makundi ya vijana kutoka nchi za Afrika ya Mashariki na nje jana, katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani, iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Vision for youth,na kufanyika katika ukumbi wa jumuiya hiyo bi Eriyo, alisema vijana wanatakiwa kujiendeleza kitaaluma ili waweze kuingia katika soko la ushindani wa ajira kwani jumuiya hiyo ipo kuwawezesha vijana kuwa huru kusafiri, kuishi na kutafuta ajira katika nchi wanachama wa jumuiya ya afrika ya mashariki .
amesema kuwa vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kufikia malengo yao, ikiwepo ya matrumizi ya madawa ya kulevya yanayopelekea kuenea kwa janga la Ukimwi na ukosefu wa taaluma inayowawezesha vijana kupata kazi kwenye mashirika ya kimataifa na kusisitiza kuwa ni jukumu la vijana sasa kujitambua na kujikwamua katika matatizo haya
Alisema kwa sasa idadi ya vijana imekuwa ikiongezeka duniani na inakadiriwa hadi kufikia 2033 idadi ya vijana itakuwa imefikia zaidi ya asilimia 60 ya watu wote wakati kwa sasa vijana waliopo katika ukanda wa jumuiya ya afrika mashariki ni asilimia sitini hali ambayo inasababisha vijana kuwa chachu ya maendeleo kwa nchi wanachama ndiyo maana jumuiya hiyo imeamua kuwekeza kwa vijana ili waweze kuleta maendeleo ktk ukanda huu wa afrika mashariki
Awali Mkurugenzi mtendaji wa shirika la vision for youth, bi Vailet Ayoub aliwataka vijana kuendelea kujiunga katika makundi ya ujasiriamali ili iwe rahisi kusaidiwa badala ya kujitenga na kulaumu serikali.
alisema vijana wana fursa za kutumia ili kujikomboa badala ya kuendelea kuilalamikia serikali hata katika mambo ambayo yapo kwenye uwezo
katika maadhimisho hayo, shirika hilo pia liliendesha shughuli za usafi katika jiji la Arusha, ikiwepo katika hospitali za serikali na kituo kikuu cha mabasi ambao ulifanywa na vijana baada ya kutembelea makao makuu ya jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Zaidi ya vijana 200 kutoka ndani na nje ya nchi walishiriki katika maadhimisho hayo ambayo yameadhimishwa kwa mara ya kwanza mkoani hapa.
Post a Comment