SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF) TAARIFA KWA UMMA


nssf f31f8
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii katika mwaka huu wa fedha linatarajia kukusanya mapato ya Tshs. Billion 706.41 kutoka kwenye michango ya wanachama ambao hadi mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu shirika lilikua na wanachama 522,763 kwa nchi nzima.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii kwa waandishi wa habari imeeleza kwamba kiasi hicho cha michango kitatokana na uandikishaji wa wanachama 169,241 wa mpango wa lazima na wanachama 85,158 wanaojiunga na NSSF kwa njia ya hiari.Katika kipindi hicho waajiri 3,062 wanatarajia kuandikishwa kwenye Shirika kuungana na waajiri 19,231 wa sasa na kufanya ongezeko la asilimia 84.07%.
Taarifa pia imeeleza kuwa kiasi cha mafao kitakacholipwa ni shilingi bilioni 199 kwa wanachama watakaoacha au kustaafu kazi katika mwaka huu wa fedha.
hdg

 
Katika mwaka huu wa fedha kiasi cha Tshs.bilioni 5.19 kitalipwa kwa ajili ya mafao ya matibabu kwa wanachama 254,399.
Wakati huo huo katika mwaka huu wa fedha,shirika linatarajia kuwekeza kiasi cha Tshs. Bilioni 951.4 ukilinganisha na Tshs bilioni 751.4 ambazo ziliwekezwa katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 sawa na ongezeko la aslimia 21.06%.
Shirika linatarajia pia kukusanya mapato ya Tshs.bilioni 181.1 kutoka kwenye vitega uchumi ukilinganisha na mapato ya Tshs bilioni 120.1 zilizokusanywa mwaka jana wa fedha. Maeneo ya uwekezaji ni pamoja na ujenzi wa daraja la Kigamboni,Dhamana za serikali,mabenki,Ubia(Listed &unlisted companies) na ujenzi wa nyumba za kuishi na biashara.
Tathmini ya thamani ya mfuko wa shirika mwaka jana ilikua Tshs.Trilioni 2.1 na thamani inatarajiwa kuongezeka na kufikia Tshs.Trilioni 2.6 katika mwaka huu wa fedha ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 19.23%.
WIKI YA NSSF
Shirika limeendelea kuadhimisha wiki ya NSSF kila mwaka kwa kushiriki katika shughuli za kijamii kwa kuendesha michuano ya vyombo vya habari ambapo michezo hiyo imetimiza mwaka wa 10 tangu ianzishwe mwaka 2004.
Mashindano hayo ambayo yameanzishwa kwa madhumuni ya kujenga mahusiano kati ya Shirika na vyombo vya habari mwaka huu yameshirikisha timu 17 za mpira wa miguu na pete ambazo zilicheza mwezi machi mwaka huu kwa muda wa wiki mbili.
Timu hizo ni NSSF yenyewe kama mdhamini, TBC, New Habari Corporation, Mwananchi, Habari Zanzibar, IPP Media,Sahara Communications, Radio Kheri, Free Media, Business Times, Uhuru/Mzalendo, Global Publishers, Tumaini Media, Changamoto, TSN, Mlimani Media na Jambo Leo.
Katika mashindano ya mwaka huu mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu ni timu ya Jambo Leo na mpira wa pete ni Business Times.
TAARIFA HII IMETOLEWA NA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF), AUGUST 21, 2013

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget