TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA BILIONI 101 KUTOKA EU

eu 8daba
Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Ulaya imetoa msaada wa hundi yenye thamani ya Yuro 47.75 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 101 kwa ajili ya kusaidia bajeti ya Serikali ili iweze kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ifikapo mwaka 2025. (HM)
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa fedha Dkt. William Mgimwa amesema fedha hizo zitasaidia katika kufikia malengo hayo ya Milenia kwa kuwa zitapelekwa kwenye uboreshaji wa huduma muhimu za jamii.
"Fedha hizi zitatumika katika kusaidia huduma muhimu za jamii ambazo zikiboreshwa zitasaidia katika kuleta maendeleo ya wananchi na hatimaye kupunguza umaskini nchini, amesema Waziri Mgimwa."
Waziri Mgimwa amefafanua kuwa fedha hizo zitatumika katika kuboresha miundombinu ya barabara, umeme, elimu, kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, vifo vya akina mama wajawazito pamoja na uboreshaji wa huduma ya maji safi.
Naye Baloz wa Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Ulaya hapa nchini Filiberto Sebregondi amesema kuwa Jumuiya hiyo imefurahishwa na jinsi Tanzania inavyojitahidi kuboresha huduma mbalimbali za jamii ili iweze kupunguza umaskini na hatimaye kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia kama ilivyopangwa.
"Fedha hizi zimekusudiwa kuisaidia Tanzania kupunguza umasikini ili iweze kufikia Malengo ya Maendelo ya Milenia ifikapo mwaka 2015", ameongeza Baloz Sebregond.
Msaada huu umetolewa ikiwa ni mwendelezo wa ahadi iliyotolewa na Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Ulaya mwaka 2009 wa kuisaidia Tanzania kiasi cha Yuro 305 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 654.7 kwa kipindi cha miaka sita na mpaka sasa jumla ya shilingi bilioni 507.7 zimeshatolewa. Chanzo: Veronica Kazimoto, Maelezo

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget