Nchini Nigeria watu wengi wamekasirishwa na tabia za baadhi ya wanasiasa ya kufuja mali na pesa za umma kwa mambo ya kidunia ambayo hupita tu, na hii ni mara baada ya kuziona picha za nyota wa R&B toka nchini humo Peter na Paul Okoye wakiwa kwenye nyumba iliyonakshiwa dhahabu inayoaminika kuwa ni ya mmoja kati ya viongozi wa Serikali ya nchi hiyo ambayo ipo kwenye Jimbo la River.
Peter Okoye aliweka picha zake na za kaka yake kwenye mitandao ya kijamii, picha zilizomuonyesha akiwa amekaa kwenye nyumba ya kifahari mara baada ya kutoka kushiriki kwenye mazishi ya mama wa Patience Jonathan yaliyofanyika ndani ya Okrika, Jimbo la Rivers.
Post a Comment