Waandishi wa habari kutoka katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha Wajitokeza kwa wingi kuchangia Damu salama

  • Katika kuhakikisha kunakuwepo na damu ya kutosha katika benki ya damu mahospitalini waandishi wa habari wametakiwa kuwa msitari wa mbele kuchangia damu pamoja na kuwafichua wale wote wanaohusika  kuuza damu kwa wagonjwa.

  • Wito huo umebainishwa na mtaalamu wa Mpango wa Taifa wa  kuchangia damu salama  Bw.George Chambo alipoongea na wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha katika zoezi  lililofanyika la uchangiaji wa damu.

  • Aidha alizitaja sifa zinazotakiwa kuwa nazo mtu kabla yakutolewa damu kuwa ni pamoja na mchangiaji lazima awe na Afya njema,asiwe na magonjwa sugu,awe mtu mwenye huruma,mwenye uzito usiopungua kilo hamsini, pamoja na wingi wa damu aliokuwa nao mwilini

  • Vilevile Bw. Chambo alisema kuwa zipofaidi za uchangiaji wa damu katika Benki ya damu kuwa ni pamoja na kujitambua kiafya ikiwepo kujua hali ya virusi vya ukimwi,kaswende pamoja na homa ya kifua kikuu.

  • Bwana Chambo amesema kuwa mpango wa kuchangia damu salama nchini tanzania niwa hiari na unamtaka kila mwenye sifa kuchangia damu katika benki  ili kila  mwenye uhitaji wakiwemo mama wajawazito, watoto chini ya miaka mitano,wanaopata ajali kupata huduma hiyo bure.

  • Hatahivyo aliendelea kusema kuwa kumekuwepo na tuhuma mbali mbali zinazowaandama madaktari na wauguzi kuhusika katika uuzaji wa damu kwa wagonjwa bilakujali uhaba uliopo katika benki hiyo bila kujali utu,wa mtu na huruma ya kibinadamu.

  • Pia Bw.Chambo alisema kuwa zipo changamoto nyingi wanazopitia ikiwepo mwitikio mdogo kwa wananchi hii ikionyosha kuwa ipo haja wananchi kupatiwa elimu juu ya umuhimu wakuchangia damu katika benki zilizopo mahospitalini.

  • habari picha,  picha zote kwa hisani ya izack boniface, izabreez.com










Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget