Sumbawanga. Nikiwa nje ya Zahanati ya Kijiji
cha Kisa kilichopo wilayani Sumbawanga
mkoani Rukwa, namuona mjamzito akiwa na
dalili za kutaka kujifungua.
Naingiwa na hofu kubwa iwapo mama huyo
atajifungua salama kutokana na mazingira
tete ya kitabibu yaliyopo kwenye zahanati hiyo,
kwani inafahamika kwamba haina wataalamu.
Hata hivyo, baada ya muda naelezwa kwamba
mama huyo amejifungua salama mtoto wa
kike, hali ambayo inanilazimu kumtafuta mtu
aliyemsaidia mama huyo kujifungua salama
kwa lengo la kujua kama naye ni mtu mwenye
ujuzi au la.
Post a Comment