Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini
amepigwa marufuku mechi mbili na UEFA
asisogelee eneo la kiufundi la uwanja kwa
kumlaumu mwaamuzi baada ya klabu yake
kushindwa na Barcelona katika michuano ya
klabu bingwa ya Ulaya.
Pellegrini alisema baada ya timu yake
kushindwa 2-0 nyumbani kwamba mwaamuzi
kutoka Sweden Jonas Eriksson "hakua
mwaadilifu kwa timu zote mbili".
Alituhumiwa kwa ukosefu wa nidhamu na
amepewa adhabu ya kukaa jukwaani pamoja
na mashabiki katika mkondo wa pili wa
mchuano na Barcelona mnamo Machi 12
March, poja na Mechi nyingine za ziada.
Adhabu ya mechi moja nyingine
imesimamishwa kwa miaka miwili.
Chanzo, bbcswahili (R.M)
Post a Comment