Baada ya Moyes kumalizana na
Man United na kuvunja mkataba,
hakuna ubishi ilikuwa ni lazima
aondoke na kwenda kupumzika
nje ya England.
Moyes alichagua Marekani, aliona
ingekuwa sehemu nzuri ambayo
angeweza kujipumzisha kabla ya
kuanza upya maisha ya
mapambano.
Kwa kuwa aliamua kwenda katika
Mji wa Florida akiwa na mkewe na
baada ya kulijua hilo, bilionea
Glazer alimpa Moyes ofa nyingine
ya kufikia katika nyumba yake ya
kifahari iliyo mjini humo.
Pia atapata huduma ya usafiri na
usimamizi wa kutembezwa
sehemu mbalimbali za jiji hilo na
wasaidizi wa Glazer.
Utaona hivi, kocha akivunja
mkataba au klabu kufanya hivyo.
Basi uadui unatangulia na
ikiwezekana viongozi wa klabu
hawataki hata kuzungumza na
kocha kwa kuwa anaonekana
kama ni adui.
Glazer ndiye anayepitisha uamuzi
wa mwisho, lakini anaonyesha
kiasi gani walivyoachana
kistaarabu na Moyes na hakuna
tatizo lolote lililotokea.
Hivyo mambo yako kitaalamu zaidi
ndiyo maana wakati mashabiki
wanaendelea kupiga kelele. Moyes
anakula ‘bata’ Marekani.
Fin.
Post a Comment