Wiki mbili zilizopita kulikuwa na
habari za matatizo/ugomvi
mkubwa katika familia ya wasanii
wa Nigeria wanaunda kundi la P-
Square, Peter na Paul. Lakini wiki
iliyoipita ilikuwa wiki ya faraja na
furaha kwa familia hiyo ambapo
matukio ya uchumba yalifunika
kombe.
Baada ya Jude Okoye, kaka
mkubwa wa P-Square ambaye pia
ni manager wao kumvisha pete ya
uchumba mpenzi wake Ifeoma
Michelle Umeokeke April 24,
mwishoni mwa wiki iliyopita
mdogo wao wa kike, Mary Okoye
pia alivishwa pete ya uchumba.
Mary Okoye alivishwa pete ya
uchumba na mpenzi wake wa
muda mrefu ambaye ni muigizaji
wa Nollywood, Emma Emordi.
Familia hiyo inayoundwa na ndugu
wenye vipaji sasa inaelekea kuwa
familia ya wana ndoa.
Mwezi March, Paul Okoye alifunga
pingu za maisha na mama mtoto
wake Anita Is
Post a Comment