June 05 2014 mchana kupitia mitandao
mbalimbali Tanzania zilisambaa taarifa
zikimuhusu mmiliki wa mojawapo ya nyumba
maeneo ya Sakina jijini Arusha kwamba
nyoka aliekua akimfuga kwa siku nyingi na
kuhusishwa na imani za kishirikina,
ameuwawa na Wananchi.
Wananchi walimuua nyoka huyo na kisha
kumkata kata vipandevipande ambapo baada
ya hizi taarifa kusambaa mmiliki wa nyumba
hii aliomba kuongea na millardayo.com ili
kutoa maelezo yake ambayo anadai ndio
ukweli wenyewe.
Mr.Joseph Paschal Magesa anasema >>Mimi
kama mimi kwanza ni Mkristo safi na mzee
wa kanisa na niliondoka nyumbani jana na
mke wangu kutoka Arusha kuelekea Dar es
salaam, sijui lolote kuhusiana na hicho kitu
ila nilipofika maeneo ya Mwanga na Same
nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka huku
ndani ya eneo la garden nyumbani, kuna
vijana niliwaacha wawili pale nyumbani
nikawaambia waambieni watu wawasaidie
kumuua huyo nyoka’
‘Wakamuita jirani yangu hapo ndipo nae
akanipigia simu nikamwambia bwana wewe si
una bunduki nisaidie kumuua huyo nyoka ila
alivyokata simu nilijua ametekeleza kumbe
aliondoka, baadae napiga tena simu nauliza
vipi naambiwa bado yupo na watu wamejaa
nikawauliza kwani hao watu hawawezi
kumuua mpaka bunduki wakasema wanaweza
ndio baadae wakanambia wamemvuta mkia
wamemuweka nje ya geti’
‘Nikawauliza anavutika asije akawa analeta
shida wakasema anavutika, nikawaambia
mpelekeni kanisani kwa sababu nyumbani
kwangu ni jirani na kanisa ndio wakamvuta
hadi kanisani wakammwagia maji ya baraka
kisha wakamkatakata ndo ikawa mwisho
wake hapo’.
‘Kusema kwamba nilikua nafuga kwamba
huyu nyoka ni mtoto wangu wa kwanza…..
sasa kama ni mtoto wangu wa kwanza si
inamaana na mtoto wangu angekufa na
yeye? mimi nasema namwachia Mungu
tu…….. sijawahi kusikia Nyoka kuishi maeneo
hayo toka nimeanza kuishi kwa karibu miaka
8, hata na mimi inanitatiza manake
nimetumiwa picha Nyoka amefungwa
kitambaa chenye maandishi mekundu kama
ya kiarabuarabu hivi…..’
‘Taarifa kwamba Nyoka huyu amevunja kioo
cha dirisha akiwa anatokea ndani ya nyumba,
sio kweli…. haipo kabisa hiyo kitu eti
kwamba ametokea ndani, hayo ni mambo ya
watu tu… hicho kioo nilikifunja mimi wakati
napanga mizigo ya ofisi yangu… sifahamu
chochote kuhusu huyu Nyoka, Watanzania
waniamini haya ninayosema ndio yanayotoka
moyoni mwangu’
Credit Millard Ayo.
Post a Comment